• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KENYA: KILIMO CHA BUSTANI KUPIGA JEKI UCHUMI WA KENYA

  (GMT+08:00) 2020-09-18 16:37:52

  Kilimo cha bustani kimepigiwa upato kufufua uchumi wa Kenya, huku taifa hili likijaribu kujikwamua kiuchumi baada ya makali ya virusi vya corona. Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na shirikia la Scope Markets, mvua nyingi ambazo zimeshuhudia katika maeneo mbali mbali nchini Kenya, zitachangia sana kufanya vizuri kwa upanzi wa mazao tofauti.

  Shirika hilo linakisia kwamba uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia 1.5 mwaka huu, mchango mkuu ukiwa hali nzuri ya ukulima wa mazao ya shambani.

  Mapato ya Kenya kutokana na mazao ya shambani na bustani yamekuwa yakuridhisha licha ya changamoto za janga la virusi vya corona.

  Kulingana na ripoti ya Shirika la Takwimu za Kitaifa, miezi saba ya kwanz aya mwaka huu, Kenya mapato ya Kenya kutoka kwa mauzo ya maua, matunda na mboga yalipanda kwa asilimia 8.6 na kufikia shilingi bilioni 93.4, pesa za Kenya.

  Akihutubia taifa tarehe 26 mwezi uliopita, rais Uhuru Kenyatta alidokeza kuwa uchumi wa taifa unaendelea vizuri, kinyume na matarajio ya wengi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako