• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Wakulima wahimizwa kutunza miundombinu ya umwagiliaji

  (GMT+08:00) 2020-09-18 16:38:37

  Wakulima nchini Zanzibar wametakiwa kuitunza miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza tija katika kilimo.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa idara ya umwagiliaji maji, Haji Hamid alipokuwa akizungumza na viongozi wa mabonde mapya yaliyowekewa miundombinu ya umwagiliaji maji.

  Aliwaomba viongozi hao kuhakikisha wanafuata maelekezo wanayopatiwa ya namna bora ya utunzaji wa miundombinu hiyo itumike kwa muda mrefu. Sambamba na hayo pia aliwataka kuwa na mwamko wa kuchangia pindi itapotokea miundombinu hiyo imeharibika na inahitaji kutengenezwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako