• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari wa ulinzi wa amani kutoka China walinda amani, kuenzi urafiki na kueneza matumaini nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-09-18 18:47:58

    Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Katika miaka 75 iliyopita, Umoja huo umechukulia amani kuwa jukumu lake, kuyachukua maendeleo kuwa lengo lake, kuchukua usawa kuwa madhumuni yake, na kutoa uhakikisho wa kimfumo kwa ajili kudumisha amani na utulivu duniani baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya dunia. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, utaratibu wa upande mmoja umefufua katika baadhi ya nchi, hali ambayo imeleta changamoto kubwa kwa utaratibu wa pande nyingi wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa. Ili kukabiliana na hali hii, na maambukizi ya virusi vya Corona, China itaendelea kuunga mkono kithabiti Umoja wa Mataifa, na utaratibu wa pande nyingi, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Hadi kufikia Septemba 17, kikundi cha kumi cha kikosi cha kulinda amani cha China nchini Sudan Kusini kimetekeleza majukumu ya kulinda amani nchini humo kwa mwaka mmoja, ambapo kimemaliza ukarabati wa barabara kuu nne na madaraja mawili yenye umbali wa kilomita 500, na majukumu zaidi ya mia moja ya kutoa misaada kwa miradi ya ujenzi.

    Ili kuhimiza mchakato wa amani nchini Sudan Kusini, na kuboresha hali ya miundo mbinu nchini humo, kikosi cha uhandisi cha kulinda amani cha China kilikwenda mji mkubwa wa pili nchini humo, Wau, kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa. Mkuu wa kikundi cha kumi cha kikosi hicho Zhang Chi anasema:

    "Miundombinu ya Sudan Kusini iko nyumba sana. Kwa mfano mjini Wau, bado hakuna mtandao wa umeme au kiwanda cha maji ya kunywa, na watoto wengi hawana nguo na viatu."

    Baada ya juhudi za miezi saba, kikosi cha uhandisi cha China kilikabiliana na matatizo mbalimbali na kukarabati barabara kuu pamoja na madaraja kabla ya msimu wa mvua, na kuboresha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wanaokaa kwenye sehemu hizo.

    Mbali na kazi ya ujenzi, askari hao waliwasaidia wakazi wa huko kuchimba visima, kutengeneza barabara za shule, kuwasaidia watoto waliojeruhiwa na kupanda mbegu ya upendo na amani nchini humo. Mwanzoni mwa mwezi Mei, baada ya kumaliza mradi wa ujenzi, askari hao walitembelea shule ya kijiji cha Sopo iliyoko karibu, na kuwazawadia watoto wa huko mpira wa soka, mabegi na vitu vingine vya utamaduni na michezo. Mkuu wa kijiji hicho Fara Barbara alishukuru kwa msaada huo kutoka kwa askari wa kulinda amani wa China. Anasema:

    "China idumu milele! urafiki kati ya Sudan Kusini na China udumu milele! Mmetusaidia kujenga upya madaraja, barabara kuu, nawakaribisheni kurudi mara kwa mara. Pia kwa niaba ya wanafunzi na shule yetu nawashukuruni, kwani vitu mlivyotuzawadia vinahitajika sana na wanafunzi, haswa mipira ya soka, ambayo imetusaidia sana."

    Mwaka uliopita, askari wa ulinzi wa amani wa China wametekeleza majukumu mbalimbali waliyopewa na Umoja wa Mataifa kwa kushinda matatizo mbalimbali, huku wakieneza matumaini ya urafiki. Katika kipindi kijacho wataendelea kukamilisha jukumu lake la kulinda amani ya dunia nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako