• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA: Kulipa kodi si lazima uwe mfanyabiashara.

    (GMT+08:00) 2020-09-21 16:41:21

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kulipa kodi si lazima mtu awe mfanyabiashara na kwamba analipa kodi kutokana na bidhaa alizonunua na kudai risiti.

    Hayo yalizungumzwa mwishoni mwa wiki jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati wa mahafali ya pili ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni wanachama wa klabu za Kodi (UDTA) zilizo chini ya mamlaka hiyo.

    Alisema kila pato analopata mtu anatakiwa kulilipia kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba ili kujiridhisha kodi imefika serikalini baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa mtu anatakiwa kudai risiti.

    Alisema lengo la kuanzisha klabu za kodi mashuleni na vyuo vikuu ni kuwezesha vijana kuwa na elimu ya kodi na kutambua umuhimu wake ambao utawafanya kuwa walipakodi wazuri wa baadae. Alisema vijana wote waliojiunga na klabu za kodi wapo katika njia sahihi kutokana na kuwa kodi ni moja ya sababu itakayoiwezesha Tanzania kuwa kama nchi za Ulaya zilizoendelea.

    Alisema ili nchi iendelee kupata mafanikio Zaidi ya haya yaliyopo sasa ni lazima TRA ikusanye mapato na kwamba ili mapato yakusanywe mamlaka inatakiwa kutoa elimu ya kodi kwa kila mwananchi na sio kuwalazimisha kulipa kodi pasipokuwa na uelewa wa umuhimu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako