• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Liverpool yang'ara mbele ya Chelsea, Sadio Mane awa shujaa wa mechi

  (GMT+08:00) 2020-09-21 16:42:26

  Liverpool wakiwa Stamford Bridge ambapo ndio nyumbani kwa Chelsea, wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli hayo yakiwekwa wavuni na Sadio Mane dakika ya 50 na 54. Baada ya ushindi huo muhimu Mane ambaye alimaliza mchezo kwa kupiga mashuti matatu tu yaliyolenga lango mawili yakiingia wavuni, yamemfanya awe mchezaji bora wa mechi hiyo. Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp, amesema wachezaji wake walipambana muda wote ndani ya uwanja mbele ya Chelsea. Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulikuwa ni wa pili kwa Liverpool kushinda baada ya kuanza kuichapa Leeds mabao 4-0. Chelsea ilikuwa ikipewa nafasi ya kufanya vizuri kutokana na usajili wao makini lakini kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki wao Andreas Christensene dakika ya 44 baada ya kumchezea faulo Mane iliwatoa kwenye ramani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako