• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mkenya Nicholas Kipkorir aandikisha muda bora mbio za Golden Spike mita 10,000

    (GMT+08:00) 2020-09-21 16:42:43

    Mkenya Nicholas Kipkorir Kimeli aliandikisha muda bora kwenye mbio za mita 10,000 mwaka 2020 baada ya kushinda makala ya 49 ya Golden Spike mjini Leiden nchini Uholanzi mnamo Septemba 19. Kimeli, 22, alimtika mizunguko 25 kwa dakika 26:58.97 na kumweka katika nafasi ya 60 kwenye orodha ya wakimbiaji 65 waliokamilisha umbali huo chini ya dakika 27. Kabla ya hapo, Benard Kibet ndiye alikuwa anashikilia muda bora mwaka huu katika mbio za mita 10,000 baada ya kutawala shindano la Fukagawa nchini Japan alipolikamilisha kwa dakika 27:14.84 akifuatwa bega kwa bega na Wakenya wenzake Bedan Karoki (27:15.97) na Jonathan Muia Ndiku (27:23.47). Rekodi ya dunia inashikiliwa na Muethiopia Kenenisa Bekele aliyetimka umbali huo kwa dakika 26:17.53 mwaka 2005. Paul Tergat (26:27.85), mwendazake Samuel Wanjiru (26:41.75), Eliud Kipchoge (26:49.02) na Geoffrey Kamworor (26:52.65).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako