• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Wanyama anatarajiwa kurejea uwanjani timu yake ya Montreal Impact ikichuana na Philadelphia Union

  (GMT+08:00) 2020-09-21 16:43:02

  Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, Victor Wanyama anatarajiwa kurejea uwanjani timu yake ya Montreal Impact ikichuana na Philadelphia Union kwenye Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) leo Septemba 21. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 amecheza dakika zote 90 katika mechi 11 tangu awasili Montreal kutoka Tottenham Hotspur nchini Uingereza mnamo Machi 3, 2020. Montreal inayonolewa na kocha Thierry Henery inashikilia nafasi ya sita kwa alama 16 baada ya kusakata mechi 11 kwenye ukanda wa Mashariki. Philadelphia iko alama tano mbele katika nafasi ya nne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako