• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mbrazil wa Simba aanza na nuksi

  (GMT+08:00) 2020-09-21 16:43:19

  Akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, kiungo mkabaji Mbrazili Gerson Fraga ameanza na nuksi baada ya kupata majeraha kwenye mchezo huo. Mbrazili alianza kucheza mchezo huo wa ligi jana, Septemba 20 wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa baada ya kumaliza ruhusa yake ya wiki mbili alizoomba kurejea nyumbani Brazil kumaliza matatizo ya familia. Kiungo huyo alikosa michezo miwili ya ligi dhidi ya Ihefu FC uliochezwa Uwanja wa Sokoine na Simba ilishinda kwa mabao 2-1 na ule dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri. Fraga alipata majeraha dakika ya tatu kabla ya kuanguka chini kutibiwa na baadaye kutolewa nje kwa ajili ya matibabu. Mbrazili huyo alitolewa nje kwa machela kwenda kupatiwa matibabu ambapo alitoka akiwa chini ya ungalizi wa jopo la madaktari. Akiwa anaendelea na matibabu nje ya Uwanja, kiungo huyo aliomba kutolewa dakika ya saba na nafasi yake kuchukuliwa na Said Ndemla.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako