• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Pep Guardiola asema atatia saini mkataba mpya na Manchester City iwapo atahisi "anastahiki"kufanya hivyo

  (GMT+08:00) 2020-09-21 16:43:38

  Kocha Pep Guardiola, 49, amesema atatia saini mkataba mpya kambini mwa Manchester City iwapo atahisi "anastahiki"kufanya hivyo badala ya kupewa tu.

  Mkataba wa sasa kati ya mkufunzi huyo raia wa Uhispania na Man-City unatarajiwa kutamatika rasmi mwishoni mwa msimu huu na ni matamanio ya usimamizi wa miamba hao kumshuhudia Guardiola akirefusha muda wake ugani Etihad. Guardiola anaanza msimu wake wa tano kambini mwa Man-City leo Septemba 21 atakapowaongoza waajiri wake kuvaana na Wolves katika gozi la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika uwanja wa Molineux. Hiki ndicho kipindi kirefu zaidi kwa Guardiola kuhudumu katika kikosi kimoja baada ya kudhibiti mikoba ya Barcelona (2008-12) na Bayern Munich (2013-16). Kwa mujibu wa Guardiola, hakuna yeyote kati ya Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak au Afisa Mkuu Mtendaji Ferran Soriano ambaye amewahi kumzungumzia kuhusu mkataba mpya. Ingawa hivyo, anahisi kwamba matarajio kutoka kwake ni ya kiwango cha juu hasa baada ya kusuasua kwao muhula uliopita ambao ulishuhudia pengo la alama 18 likitamalaki kati yao na mabingwa Liverpool.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako