• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajiwa kuchangia zaidi uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-09-21 17:01:29

    Mwaka huu China imeweka mpango wa kujenga muundo mpya wa maendeleo unaozingatia mizunguzo miwili ya ndani na ya kimataifa. Mpango huo ni uamuzi wa kimkakati wa kuelekeza maendeleo ya kiuchumi ya China katika siku zijazo.

    Mkuu wa heshima wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Lin Yifu anaona kuwa, muundo mpya wa maendeleo umepangwa kutokana na mabadiliko yanayoshuhudiwa katika kiwango, mazingira na hali ya maendeleo ya China. Mpango huo ni uamuzi wa kimkakati wa kujenga upya ushirikiano wa kimataifa na nguvu bora ya ushindani ya China, ni chaguo la lazima na pia ni chaguo la kunufaishana.

    Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Biashara Duniani WTO, mwaka huu biashara ya kimataifa inatarajiwa kupungua kwa asilimia 13 hadi asilimia 32, punguo ambalo huenda litazidi lile lililoshuhudiwa mwaka 2008 kutokana na msukosuko wa kifedha wa kimataifa. Katika mazingira ambayo mahitaji ya kimataifa yanaendelea kushuka, China inapaswa kuharakisha juhudi za kuchochea matumizi ya ndani na kuongeza msukumo kwenye mzunguko mkubwa wa ndani.

    Ikilinganishwa na changamoto ya kipindi kifupi, ni muhimu zaidi kutupia macho kipindi kirefu cha baadaye. Bw. Lin Yifu anaona kuwa, zamani maendeleo ya China yalitegemea zaidi soko la kimataifa, kutokana na kuongezeka kwa uchumi na kurekebishwa kwa muundo wa uchumi, utegemezi wa China kwa soko la ndani umeongezeka siku hadi siku. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2019, matumizi ya ndani yalichangia asilimia 57.8 ya ukuaji wa uchumi wa China, na yamekuwa msukumo wa kwanza wa ukuaji wa uchumi kwa miaka sita mfululizo.

    Bw. Lin Yifu amesema, katika miaka ya karibuni, China imedumisha mchango wa asilimia 30 kwa ukuaji wa uchumi wa dunia, na chini ya muundo mpya wa maendeleo, China inayofungua mlango zaidi kwa nje inatarajiwa kuchangia zaidi uchumi wa dunia.

    Mwaka jana miongoni mwa kampuni 494 za Unicorn duniani, kampuni 206 ni za China, idadi ambayo inachukua nafasi ya kwanza duniani.

    Bw. Lin Yifu anaona kuwa, China kujenga muundo mpya wa maendeleo, kamwe hakumaanishi inafunga mlango wake. Wakati China inachochea mahitaji ya ndani na kuhimiza uvumbuzi, pia itaendelea kuinua kiwango cha kufungua mlango kwa nje na kujenga mazingira bora ya nje, ili iweze kutumia vizuri masoko mawili ya ndani na ya kimataifa, na raslimali za aina mbili. Ameongeza kuwa, kwa kufanya hivyo, China itaweza kuendelea kupata fursa za soko na ushirikiano, na kuzinufaisha nchi rafiki kutokana na utandawazi na maendeleo ya uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako