• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchukua hatua kufuatia maofisa waandamizi wa Marekani kufanya ziara kisiwani Taiwan

    (GMT+08:00) 2020-09-21 21:07:48

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, China itachukua hatua halali kufuatia maofisa waandamizi wa Marekani kufanya ziara kisiwani Taiwan, pamoja na hatua dhidi ya watu binafsi wanaohusika.

    Wang ameihimiza Marekani iache mawasiliano yoyote rasmi na Taiwan, na kusema ziara hizo zimekiuka sera ya kuwepo kwa China moja, na taarifa tatu za pamoja za nchi hizo mbili.

    Habari zinasema naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Keith Krach alifanya ziara huko Taiwan wiki iliyopita, na kukutana na kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen, baada ya waziri wa afya na huduma za kibinadamu wa Marekani Alex Azar kuzuru kisiwa hicho mwezi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako