• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 75 tangu Umoja wa Mataifa kuanzishwa

    (GMT+08:00) 2020-09-22 09:08:47

    Rais Xi Jinping wa China jana amehutubia Mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.

    Katika hotuba yake, Rais Xi amesisitiza kuwa, baada ya maambukizi ya virusi vya Corona kumalizika, Umoja huo unapaswa kuwa na haki, kushikilia utekelezaji wa sheria, kuhimiza ushirikiano na kuzingatia utekelezaji. Pia amesisitiza kuwa, China ni nchi ya kwanza kusaini katiba ya Umoja wa Mataifa, ni nchi mwanachama mwanzilishi wa Umoja huo, pia ni nchi pekee inayoendelea iliyo mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    "China siku zote inatekeleza uratibu wa pande nyingi, kujitahidi kushiriki kwenye mageuzi na ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa dunia, kushikilia kulinda mfumo wa kimataifa unaotegemea Umoja wa Mataifa, kulinda utaratibu wa kimataifa wenye msingi wa sheria ya kimataifa, na kulinda umuhimu wa umoja huo katika mambo ya kimataifa."

    Rais Xi amesisitiza kuwa, dunia iko katika mwanzo mpya wa kihistoria, na kurejea tena ahadi ya kuwa na uratibu wa pande nyingi, kusukuma mbele kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu, na kutimiza mshikamano na maendeleo makubwa zaidi chini ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako