• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mbwana Samatta kuijunga na Fenerbahce kwa mkopo

  (GMT+08:00) 2020-09-22 15:35:18

  Baada ya Mzee Ally Pazi kutoa baraka zote kwa mwanawe, Mbwana Samatta kufanya maamuzi kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Uturuki, imeripotiwa kuwa nahodha huyo wa Taifa Stars amekubali kujiunga kwa mkopo wa muda mrefu na Fenerbahce. Kwa mujibu wa gazeti la Takvim huko nchini Uturuki, imeripotiwa kuwa Aston Villa klabu ambayo anaichezea Samatta na Fenerbahce wamefikia makubaliano ambayo yatamfanya mshambuliaji huyo kuitumikia miamba hiyo ya Uturuki kwa mkopo wa msimu mzima. Imeelezwa mkopo huo utakuwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja mara baada ya kumalizika mwakani. Mkataba wa Samatta na Aston Villa ambayo alijiunga nayo kwa Pauni 8.5 millioni mwanzoni mwa mwaka huu (Januari), unatarajiwa kumalizika mwaka 2024. Ripoti hiyo, ilieleza Samatta anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Fenerbahce ambacho wikiendi ijayo kitacheza dhidi ya Galatasaray ambayo aliwahi kuichezea Muafrika mwenzake, Didier Drogba. Awali Besiktas ambayo na yenyewe ni klabu kutoka Uturuki iliripotiwa kuongoza mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Tanzania ambaye ameripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamewekwa sokoni na klabu yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako