• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Liverpool yainyemelea saini ya Mbappe

  (GMT+08:00) 2020-09-22 15:35:44

  Imeripotiwa kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye hesabu za kumpata mshambuliaji wa Klabu ya Paris Saint-German, (PSG) Kylian Mbappe kwa ajili ya kuibukia ndani ya kikosi hicho ambacho kinatetea taji la Ligi Kuu England. Saini ya Mbappe raia wa Ufaransa pia inawindwa na Klabu ya Real Madrid jambo ambalo linaongeza ushindani kwa timu hizi mbili kubwa kupambana kupata saini yake. Mbappe bado ana mkataba na PSG kwa kuwa amebakiza dili la miaka miwili lakini kuna kipengele cha kufanya makubaliano na timu ambayo inahitaji saini yake. Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Ufaransa la L'Equipe ni kuwa Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anamtazama kwa ukaribu Mbappe ili kumuongeza ndani ya kikosi chake na kumng'oa ndani ya Ligue 1 ili ashiriki Ligi Kuu England.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako