• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Manchester City Kelvin yairarua Wolves 3-1 ligi kuu England

  (GMT+08:00) 2020-09-22 15:36:15

  Nyota wa Manchester City Kelvin De Bruyne alifungua pazia la ushindi wakati timu yake ikishinda mabao 3-1 mbele ya Wolves kwenye mchezo wa Ligi Kuu England England uliochezwa usiku wa kuamkia leo dakika ya 20 kwa mkwaju wa penalti. Mabao mengine yalifungwa na Phili Foden dakika ya 32 kisha Wolves walipata bao la kufutia machozi dakika ya 78 kupitia kwa Raul Jimenez na msumari wa mwisho wa Manchester City ukipachikwa kimiani na Gabriel Jesus dakika ya 90. Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola ilionekana kuwa bora kwenye mchezo huo licha ya kuwa ugenini Uwanja wa Molineux kwa kuwa ilimiliki mpira asilimia 66 huku wapinzani wao wakimiliki asilimia 34. Guardiola amesema kuwa timu ilikuwa tayari na ilianza vizuri kipindi cha kwanza jambo lilowapa matokeo mazuri kwenye mchezo wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako