• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika wajadili hotuba ya Rais Xi Jinping aliyotoa kwenye Mkutano wa Kuadhimiaka Miaka 75 ya UM

    (GMT+08:00) 2020-09-22 18:18:40

    Rais Xi Jinping wa China jana Jumatatu alitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa kilele wa Kuadhimisha Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Wataalamu wa nchi mbalimbali za Afrika wakijadili hotuba ya Rais Xi, wameeleza kukubali mapendekezo aliyotoa kwenye hotuba hiyo, na kuona kuwa hotuba hiyo imeongeza imani na msukumo kwa jumuiya ya kimataifa katika kutekeleza taratibu za pande nyingi na kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

    Mtafiti wa Kituo cha Utafiti wa Mawasiliano ya Kiuchumi na Kiutamaduni kati ya China na Afrika cha Zimbabwe Bw. Donald Rushambwa amesema, China na nchi za Afrika ikiwemo Zimbabwe zote ni watetezi na walinzi wa taratibu za pande nyingi. Katika dunia ya utandawazi, nchi nyingi zinakubaliana kuwa sera za upande mmoja ni njia isiyopitika. Amesema msimamo wa China wa kulinda taratibu za pande nyingi ni muhimu sana. Wakati mwelekeo wa dunia wa mfumo wenye ncha nyingi unaonekena kidhahiri, kila nchi inatumai kuwa na sauti zaidi kwenye usimamizi wa dunia, na kujenga utaratibu wa kimataifa wenye mfumo wa pande nyingi kuwa kiini chake kunalingana na maslahi ya nchi nyingi duniani. Bw. Rushambwa anaona kuwa janga la virusi vya Corona linaloenea dunia nzima, limeonesha haja na ulazima wa kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

    Mtaalamu wa mambo ya kimataifa wa Kenya Bw. Cavince Adhere ameeleza kuyakubali mapendezo manne aliyotoa Rais Xi Jinping kuhusu jinsi Umoja wa Mataifa utakavyatekeleza majukumu yake baada ya janga la virusi vya Corona kumalizika. Amesema, China inachukua nafasi muhimu katika masuala ya kimataifa, na umuhimu wake unaonekana wazi katika juhudi zake za kutetea taratibu za pande nyingi na kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa. Amesema, mwitikio wa dunia kwa janga la virusi vya Corona umeonesha kuwa mustakbali na hatma ya binadamu wote ni ya pamoja, kwa hivyo nchi zote duniani zinapaswa kuimarisha mshikamano na kuzidisha ushirikiano, ili Dunia iweze kuendelea kupiga hatua mbele.

    Mkurugenzi wa kitivo cha lugha ya kichina katika chuo kikuu cha Cairo Rehab Mahmoud amesema, China imefanya jitihada kubwa katika kulinda taratibu za pande nyingi, na pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China ndio ni moja ya hatua muhimu za kutekeleza utaratibu wa pande nyingi. Amesema anaamini kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi katika kulinda taratibu hizo chini ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.

    Naye mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Masuala ya China cha Nigeria Bw. Charles Onunaiju amesema, China inalinda kithabiti taratibu za pande nyingi, na kulinda kihalisi maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa kupitia juhudi zake katika operesheni za kulinda amani, kupambana na maharamia, na kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na milipuko ya Ebola na virusi vya Corona. Amesema pendelezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China ni mpango wa kutimiza lengo la kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja, na pia ni ahadi mpya ya China ya kulinda taratibu za pande nyingi katika mwanzo mpya wa kihistoria, ili nchi mbalimbali ziweze kuwasiliana na kushirikiana kwa ufanisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako