• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa CMG atoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa dhidi ya janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-22 19:19:19

    Jumuiya ya Kimataifa ya Mashirika ya Televisheni ya Njia ya Hariri iliyoanzishwa na Kampuni Kuu ya Kimataifa ya Televisheni ya China iliyoko chini ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG imeanzisha "harakati ya mapendekezo ya utendaji wa majopo ya washauri bingwa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kujenga afya ya Njia ya Hariri". Harakati hiyo imeitikiwa na washauri bingwa na wataalamu wengine wenye ushawishi, ambao wametoa mapendekezo mbalimbali, na kutaka jumuiya ya kimataifa kujizatiti zaidi na kuongeza ushirikiano, ili kutoa uungaji mkono wa kiakili kwa juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19.

    Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye pia ni mkuu wa CMG Shen Haixiong ametoa salamu kwa harakati hiyo, akitaka vyombo vya habari duniani vijitolee, kuzidisha ushirikiano, kuripoti ukweli, na kujenga maoni sahihi, ili kuchangia juhudi za kimataifa za kupambana na janga la COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako