• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapendekezo ya rais Xi Jinping yapongezwa na jamii ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-09-22 19:19:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, akitoa mapendekezo manne kuhusu aina gani ya Umoja wa Mataifa dunia inayohitaji, na jinsi Umoja huo utakavyofanya kazi baada ya janga la COVID-19. Mapendekezo hayo ya Rais Xi yamepongezwa na jamii ya kimataifa.

    Wang amesema mapendekezo hayo yametoa alama dhahiri ya China kulinda mfumo wa kimataifa wenye Umoja wa Mataifa kuwa kiini chake, kulinda utaratibu wa kimataifa wenye sheria ya kimataifa kuwa msingi wake, kulinda taratibu za pande nyingi, kushiriki kwenye mageuzi na ujenzi wa usimamizi wa mambo ya kimataifa, na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako