• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawakilisha nchi 80 kutoa wito wa kuondoa umaskini na kuhimiza ulinzi wa haki za binadamu

    (GMT+08:00) 2020-09-23 09:22:43

    Balozi wa China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Chen Xu ameziwakilisha nchi 80 za Asia, Afrika na Latin America kutoa ripoti ya kupunguza umaskini na kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu kwenye Mkutano wa 45 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo.

    Balozi Chen amesema, kuondoa umaskini ni lengo muhimu la kwanza katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, ambayo pia ni njia muhimu ya kuhimiza na kulinda haki za binadamu. Hivi sasa, watu milioni 800 ni maskini na wengine milioni 71 watarudi kwenye umaskini kutokana na janga la virusi vya Corona, hali itakayoendelea kuharibu usawa wa jamii.

    Balozi Chen pia amesema, nchi mbalimbali zinapaswa kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza umaskini. Nchi zilizoendelea zinatakiwa kutoa misaada ya kupunguza umaskini na ya kiufundi kwa nchi zinazoendelea na nchi zilizo nyuma kimaendeleo. Pia amehimiza pande zote kubadilishana uzoefu na njia nzuri katika kuondokana na umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako