• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahutubia mjadala wa kawaida wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-09-23 09:31:21

    Rais Xi Jinping wa China jana amehutubia mjadala wa kawaida wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China itaendelea kubadilishana uzoefu wake katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na teknolojia ya matibabu, kuunga mkono na kutoa msaada kwa nchi zinazohitaji, kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa ugavi wa vifaa vya mapambano dhidi ya virusi vya Corona duniani, na kushiriki kwenye utafiti wa kutafuta chanzo na njia za kuenea kwa virusi hivyo.

    Amesema kuwa, chanjo kadhaa za China zimeanza kufanyiwa majaribio ya kipindi cha tatu, na zitakuwa bidhaa za umma baada ya kutimizwa utafiti, na kutoa kipaumbele kwa matumizi yake katika nchi zinazoendelea.

    Rais Xi pia ametangaza kuwa, ili kuunga mkono umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika mambo ya kimataifa, China itatoa dola za kimarekani milioni 50 kwa mpango wa kibinadamu wa Umoja huo katika kukabiliana maambukizi ya virusi vya Corona, kuweka dola za kimarekani milioni 50 katika mfuko wa ushirikiano wa Kusini na Kusini, kuongeza miaka mitano mingine ya Mfuko wa Amani na Maendeleo kati ya China na Umoja wa Mataifa baada ya muda wake kumalizika mwaka 2025. China pia itaanzisha Kituo cha Umoja wa Mataifa cha habari za kijiografia na uvumbuzi duniani na Kituo cha utafiti wa data kubwa za maendeleo endelevu, ili kutoa msukumo mpya katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako