• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya Corona Marekani yazidi laki 2

    (GMT+08:00) 2020-09-23 18:41:46

    Hadi kufikia tarehe 22, idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya Corona nchini Marekani ilizidi laki 2. Shirika la habari la CNN lilitoa habari likisema kuwa, tangu mtu wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Corona agunduliwe Februari 6 nchini Marekani, wastani wa watu 858 wanakufa kutokana na virusi hivyo kila siku.

    Habari zinasema, idadi hiyo imezidi ile ya jumla ya wamarekani waliokufa katika vita 5 vya karibuni.

    Wachunguzi wanakadiria kuwa, hadi kufikia Januari mosi mwakani, huenda wengine karibu laki 1.8 watakufa kutokana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako