• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wafanyakazi wa posta watengewa fedha kuwalipa mishahara

    (GMT+08:00) 2020-09-23 18:55:50

    Wizara ya fedha nchini kenya imeidhinisha Shilingi milioni 810 kwa malipo ya malimbikizo ya mishahara ya miezi sita ya wafanyikazi wa Shirika la Posta (PCK).

    Uamuzi huo umekuja baada ya wafanyikazi hao kuomba Bunge kuingilia kati baada ya shirika hilo la serikali kutowalipa tangu Machi, wakati janga la Covid-19 liliripotiwa nchini.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara hiyo bibi Esther Koimett ameambia kamati ya leba ya Bunge kuwa wizara hiyo imetenga kiasi hicho kwa shirika hilo.

    Shirika halijalipa wafanyikazi wake zaidi ya 2,000 tangu Machi na na linasema halikapata fedha zozote kutokana na janga la corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako