• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Benki zatakiwa kuanisha ada za utoaji pesa kwa ATM

    (GMT+08:00) 2020-09-23 18:56:41

    Benki Kuu ya Uganda inataka benki za kibiashara zianze kutoza kiwango sawa cha ada kwa wateja wanaotumia ATM kama sehemu ya mpango wa kukuza oparesheni kidijitali

    Akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na Chama cha Mabenki cha Uganda (UBA) , mkurugenzi wa mifumo ya malipo ya kitaifa ya Benki kuu ya Uganda Bwana Mackay Aumo, alisema kuanisha ushuru unaotozwa kwenye ATM ni muhimu katika kuhamasisha malipo ya dijitali.

    Alisema lazima benki zizingatie tena kuanisha ada, ambayo alibaini, kuwa ina faida zaidi.

    Naye naibu gavana wa Benki kuu ya Uganda Bwana Micheal Atingi-Ego, alisisitiza hitaji la uanishaji kukuza shughuli za dijitali, lakini akasema kwamba hatua hiyo itategemea utayari wa benki za biashara.

    Ada za kutoa pesa kwa kutumia ATM kulingana na taakwimu zilizotolewa na Benki Kuu mwezi Januari ni kati ya Shilingi 600 na Shilingi 1,500.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako