• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Watatu West Ham United wakutwa na corona akiwemo kocha wao

  (GMT+08:00) 2020-09-23 19:03:58

  Klabu ya West Ham United imethibitisha kuwa kocha wao David Moyes, beki wao Issa Diop na kiungo Josh Cullen wamepata maambukizi ya virusi vya Corona. Taarifa hizo zimetoka muda mchache kabla ya mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Hull City, hivyo Diop, Moyes na Josh Cullen wakaondolewa mapema katika orodha ya watakaoshiriki. Kocha msaidizi wa West Ham United Alan Irvine ndio alikiongoza kikosi cha West Ham United katika mchezo wa round ya tatu wa Carabao dhidi ya Hull City na West Ham kupata ushindi wa magoli 5-1. Wakati huohuo klabu ya Man United imeifunga klabu ya Luton katika michuano ya Carabao Cup kwa ushindi wa magoli 3-0. Magoli ya Man United yalifungwa na Anthony Martial kwa mkwaju wa penati dakika ya 44, Marcus Rashford dakika ya 88 na goli la mwisho likifungwa dakika mbili za nyongeza na Greenwood. Kwa matokeo hayo sasa ni wazi Man United wanasonga mbele katika hatua ya round ya nne ambapo watacheza na mshindi wa mchezo wa Preston North End dhidi ya Brighton.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako