• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakataa na kukanusha vikali shutuma zisizo na msingi za Marekani kwenye UM

    (GMT+08:00) 2020-09-23 19:15:06

    China imekataa na kukanusha vikali shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na Marekani wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa UM, na kusema itatumia haki yake ya kujibu kwa mujibu wa sheria za baraza kuu kueleza msimamo wake.

    Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun. Amesema lawama za Marekani haziendani na mazingira ya mkutano mkuu, kwani wakati jamii ya kimataifa inajadili mapambano dhidi ya COVID-19, Marekani inasambaza virusi vya siasa. Halkadhalika wakati jamii ya kimataifa inapohitaji zaidi mshikamano na ushirikiano, Marekani inatumia vibaya jukwaa la Umoja wa Mataifa kuanzisha makabiliano na kuleta mgawanyiko. Zhang pia amesema wakati jamii ya kimataifa inahitaji Umoja wa Mataifa ulio imara, Marekani inaudhoofisha umoja huo pamoja na mashirika yake likiwemo Shirika la Afya Duniani, pamoja na kudhoofisha mamlaka na ufanisi wa UM.

    Zaidi ya viongozi 120, rais wa Baraza Kuu na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa wameongea kwenye mkutano mkuu, wakitoa wito kwa nchi mbalimbali kujitahidi kushikilia taratibu za pande nyingi, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kukabiliana kwa pamoja na changamato za dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako