• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vikali uongo wa Marekani katika UM, na kutoa wito wa kuacha mchezo wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2020-09-23 19:32:23

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema China inapinga vikali uongo na shutuma zisizo na msingi dhidi yake zilizotolewa na Marekani kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambazo zinatokana na sababu za kisiasa.

    Akijibu kauli zilizotolewa na rais Donald Trump dhidi ya China kwenye mkutano mkuu wa 75 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Wang Wenbin amesema ukweli umethibitisha kwa mara nyingine tena kwamba vitendo vya upande mmoja na mabavu ni matishio makubwa yanaoikabili dunia. Amesema uongo hauwezi kubadilisha ukweli, kwani juhudi za mwitikio wa COVID-19 za China zimerikodiwa, na watu watahukumu kwa haki, akiongeza kuwa China imeripoti janga, kutambua kisababishi cha ugonjwa na kutangaza muundo wa jeni za virusi vya Corona muda mfupi baada ya janga hilo kutokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako