• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafanikio ya China kukabiliana na COVID-19 yatokana na hatua madhubuti za serikali na uungaji mkono wa wananchi

    (GMT+08:00) 2020-09-23 20:25:29

    China imepata mafanikio makubwa katika kukabiliana na janga la COVID-19, ambapo uzalishaji wa sekta mbalimbali za uchumi umerejeshwa, na wanafunzi wamerejea mashuleni na vyuo vikuu. Vyombo vya habari vya nchi za nje vinaona kuwa, mafanikio hayo yanatokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na serikali ya China dhidi ya virusi vya Corona, na uungaji mkono wa wananchi wake.

    Gazeti la News Week la Marekani limetoa ripoti, ikisema mwezi uliopita mkusanyiko mkubwa wa watu kwenye bwawa la kuogelea mjini Wuhan ulishangaza watu wengi duniani, na kuonesha kuwa hali ya China ni tofauti sana na ile ya Marekani na India ambazo bado zinasumbuliwa vibaya na janga la COVID-19. Ripoti hiyo inasema China imefanikiwa kudhibiti virusi vya Corona, kutokana na utekelezaji wa hatua madhubuti na imani ya wananchi kwa serikali yao.

    Gazeti la Bangkok Post la Tailanda limesema, China imefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya miezi mitatu, hali hii inatokana na uongozi imara wa serikali, mfumo kamili unaoshirikisha pande zote wa kukabiliana na virusi, na uungaji mkono mpana wa wananchi. Ikilinganishwa na China, serikali ya Donald Trump ya Marekani ni dhaifu katika kukabiliana na janga la COVID-19, hivyo Marekani imekuwa nchi iliyopata pigo kubwa zaidi la janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako