• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China na katibu mkuu wa UM wakutana kwa njia ya video

    (GMT+08:00) 2020-09-24 09:11:35

    Rais Xi Jinping wa China jana jioni amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres kwa njia ya video.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China inashikilia kuunga mkono umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika mambo ya kimataifa, na kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa. Amesema China inapenda kubadilishana uzoefu wake na pande mbalimbali katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, na kuendelea kuunga mkono na kutoa msaada kwa nchi zenye mahitaji. Rais Xi ameongeza kuwa, China inaunga mkono uongozi wa mfumo wa Umoja wa Mataifa hasa WHO, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kinga na udhibiti kwa pamoja, na kujenga jumuiya ya pamoja ya afya ya umma. China pia itatimiza ahadi yake, kuifanya chanjo iwe bidhaa za umma kwa dunia nzima ili kutoa mchango kwa ajili ya kupatikana na kumudu katika nchi zinazoendelea.

    Kwa upande wake, Bw. Guterres amesema, hivi sasa dunia inakabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, mabadiliko ya hali ya hewa na changamoto nyingine, hivyo inahitaji uratibu wa pande nyingi, ushirikiano wa kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa wenye nguvu zaidi. Ameishukuru China kwa kuunga mkono uratibu wa pande nyingi na Umoja wa Mataifa, na kusema China imechukua nafasi muhimu katika kulinda amani na kutekeleza maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako