• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UHAMISHO: Luis Suarez sasa rasmi anatinga Atletico Madrid

  (GMT+08:00) 2020-09-24 17:41:22

  Klabu za FC Barcelona na Atletico Madrid zote leo zimetangaza kuafikiana juu ya uhamisho wa mchezaji Luis Suarez kuwa sasa anahamia Atletico Madrid kwa kiasi kinachotajwa kufikia euro milioni 6. Wakati wowote kuanzia sasa baada ya Luis Suarez kupima vipimo vya afya atatangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Atletico Madrid, hiyo ni baada ya kuwa nje ya mipango ya kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman. Kabla ya uhamisho huo Suarez baada ya kuthibitika kuwa anaondoka Barcelona, chaguo lake la kwanza lilikuwa ni kwenda kucheza soka Italia katika klabu ya Juventus ila kutokuwa mchezaji anayetoka nchi za umoja wa Ulaya (EU) na kushindikana kupata uraia kumekwamisha dili hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako