• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TUZO: Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakosekana tatu bora tuzo za UEFA

    (GMT+08:00) 2020-09-24 17:42:48

    Katika hali isiyo ya kawaidi huwezi kutarajia kuwa msimu wa mwaka 2019/20 wachezaji ghali, bora kabisa duniani na wenye mafanikio makubwa kwenye soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wasingeliweza kukosekana hata tatu bora katika tuzo za mchezaji bora wa mwaka zinazotolewa na UEFA. Lakini hilo limewezekana, baada ya Jumatano UEFA kutoa orodha ya majina matatu ya wachezaji ambayo ndiyo yameingia kwenye tatu bora kuwania tuzo hiyo na kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya Mwongo mmoja kupita majina maarufu na yaliyozoeleka katika kuzichukua tuzo hizi, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekosekana. Majina ya wachezaji Robert Lewandowski na Manuel Neuer kutokea Bayern Munich, na la tatu likiwa ni la kijana wa Manchester City, Kevin De Bruyne ndiyo yaliobahatika kuingia tatu bora na hatmaye kupatikana mchezaji bora wa mwaka kwenye tuzo zitakazotolewa siku ya Alhamisi ya tarehe 1 Oktoba. Nyota huyo wa Barcelona, Messi ametwaa tuzo hizo katika mwaka 2010-11 na 2014-15 na jina lake limeingia kwenye kinyang'anyiro hicho zaidi ya mara sita ndani ya misimu 10. Wakati kwa upande wa Ronaldo amejibebea tuzo hiyo zaidi ya mara tatu 2013-14, 2015-16 na 2016-17 na kipindi chote hicho alikuwa akikitumikia kikosi cha Real Madrid. Na ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho zaidi ya mara tisa, na kwenye msimu wa 2017-18 aliingia hadi kwenye nafasi ya pili na mara tano akishika nafasi ya tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako