• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba yazifunika timu za Afrika kwa kushika namba moja kwenye Mtandao wa Istagram

  (GMT+08:00) 2020-09-24 17:43:09

  Klabu ya Simba imezifunika timu nyingi Afrika ikiwa ni pamoja na Klabu ya Al Ahly ya Misri kutokana na kushika namba moja kwenye Mtandao wa Istagram. Hiyo ni kwa mujibu wa Mtandao wa Deporfinanzas ambao umetoa takwimu za mwezi Agosti na kuiweka Simba namba moja kwa umaarufu kutokana na kutembelewa sana na watu. Takwimu zinaonyesha kwamba kwa mwezi huo watu milioni 536 waliitembelea akaunti ya Simba huku ile ya Al Ahly ilitembelewa na watu milioni 517 na Raja Casablanca watu milioni 511. Hii ni mara ya Kwanza kwa timu kutoka Tanzania kufanya hivi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako