• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Nyota wa NBA huenda wasishiriki Olimpiki jijini Tokyo Japan

  (GMT+08:00) 2020-09-24 17:45:14

  Kamishna wa mchezo wa kikapu nchini Marekani NBA, Adam Silver amesema kuna uwezekano wachezaji nyota nchini humo kutoshiriki mashindano ya Olympic jijini Tokyo Japan mwezi Julai. Silver ametoa kauli hiyo kutokana na uwezekano wa muingiliano wa ratiba hizo mbili ambapo Silver amenukuliwa akisema msimu wa NBA hautokuwa tena mwezi Disemba badala yake utaanza mwezi Januari 2021 hii inamaanisha hatua ya mtoano itaisha ndani ya mwezi Agosti au Septemba. Michuano ya Olympic hukusanya wachezaji wa ligi mbalimbali duniani ikiwemo NBA ambao huwakilisha mataifa yao. Aidha Silver amesema nyota 15 bora wa NBA huweza wasishiriki michuano ya Olympic ingawa wengine waliosalia wataendelea kuwakilisha mataiafa yao. Ratiba ya shughuli mbalimbali duniani ikiwemo michezo imeathiriwa kwa kiwango kikubwa hii ni kufuatia dunia kukumbwa na janga la CORONA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako