• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ahadi aliyoitoa Rais wa China kwenye mkutano wa Baraza kuu la UM yatia moyo mwitikio wa dunia kwa mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2020-09-24 18:33:28

    Rais Xi Jinping wa China juzi jumanne alitoa hotuba muhimu kwenye mjadala wa kawaida wa kikao cha 75 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, na mambo aliyoyataja kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yamefuatiliwa na kujadiliwa na vyombo vya habari vya kimataifa. Baadhi ya wataalamu wa nchi za magharibi wanaona kuwa ahadi ya China imetia moyo kwenye mwitikio wa dunia kwa mabadiliko ya tabianchi.

    Kwenye hotuba yake Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi ambayo yanawakilisha mwelekeo wa dunia wa kuelekea uchumi wa kaboni pungufu, ni hatua za kikomo cha chini zinazotakiwa kuchukuliwa na nchi zote ili kulinda Dunia yetu. Amesema China itachukua hatua na sera zenye nguvu zaidi, ili kufanya kiwango cha utoaji wa gesi ya ukaa kifikie kilele kabla ya mwaka 2030, na kujitahidi kutimiza lengo la utoaji sifuri wa gesi ya ukaa kupitia uwiano kati ya utoaji na unyonyaji wa gesi hiyo (Carbonneutral), kabla ya mwaka 2060.

    Shirika la habari la Ufaransa AFP lilimnukuu mtaalamu wa tabianchi wa Chuo cha Imperi London Dkt. Joeri Rogelj akisema kuwa ahadi hiyo ya China ni muhimu sana, na itatia moyo katika mwitikio wa dunia nzima dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

    Naibu mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Raslimali za Dunia Helen Mountford amesema, ahadi hiyo ya China itatoa athari kubwa chanya kupitia nyanja ya diplomasia, na itaongeza imani ya nchi nyingine zinazotoa gesi ya ukaa kwa wingi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    Mwenyekiti wa Mfuko wa Tabianchi wa Ulaya Bi. Laurence Tubiana kutoka Ufaransa ambaye alishiriki kwenye utungaji wa Makubaliano ya Paris, alisema mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi utafanyika mwakani, na juhudi zinazofanywa na viongozi wa China, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine nyingi zinazoendelea zimetutia moyo watu wote.

    Rais wa Tume ya Ulaya Bi. Ursula Von Der Leyen jana aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakaribisha mpango na lengo lililotolewa na China, na kusema hii ni hatua muhimu katika mwitikio wa dunia kwa mabadiliko ya tabianchi chini ya mfumo wa Makubaliano ya Paris, na Umoja wa Ulaya utashirikiana na China ili kutimiza lengo hilo.

    Gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti kuwa katika mazingira ambayo janga la virusi vya Corona limesababisha uharibifu mkubwa kwa uchumi na jamii kote duniani, ahadi ya dhati iliyotolewa na China itatoa msukumo mpya kwa juhudi za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    Shirika la habari la Marekani AP limetoa ripoti likisema hivi sasa nchi zipatazo 30 ikiwemo China zimetoa ahadi ya utoaji sifuri wa gesi ya ukaa kupitia Carbonneutral, na nchi hizo zinachangia asilimia 43 ya utoaji wa Dioksidi kabonia kutokana na matumizi ya nishati ya visukuku. Lakini Marekani, India, Australia na nchi nyingine zinazotoa hewa ya ukaa kwa wingi bado hazijajiunga na ahadi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako