• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi mbalimbali zalaani vikwazo vya upande mmoja vya Marekani katika Baraza la haki za binadamu la UM

    (GMT+08:00) 2020-09-24 19:22:54

    Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Septemba 22 kwenye Mkutano wake wa 45 lilifanya mazungumzo na mwakilishi maalumu wa Umoja huo wa kuchunguza athari hasi za hatua za upande mmoja kwa haki za binadamu, ambapo wajumbe wa nchi nyingi walilaani vikali vikwazo vya upande mmoja vya Marekani ambavyo vilisababisha watu wa nchi zilizowekewa vikwazo kutoweza kupata vitu na huduma za msingi, na kukiuka haki za binadamu pamoja na kukwamisha maendeleo ya uchumi na jamii.

    Mjumbe wa China alisema, hatua za vikwazo vya upande mmoja vikiwemo vizuizi vya kiuchumi na kifedha, zilizochukuliwa na nchi fulani ziliathiri vibaya utaratibu wa siasa na uchumi wa kimataifa na mfumo wa usimamizi wa dunia, huku zikidhuru uwezo wa nchi zilizowekewa vikwazo wa kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu wake, na kusababisha ukiukaji endelevu wa kimfumo dhidi ya haki za binadamu. Baraza la haki za binadamu na mwakilishi maalumu wanapaswa kuihimiza nchi husika iondoe hatua hizo za upande mmoja na kuacha kukiuka haki za binadamu za watu wa nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako