• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumko wa bei washuka Zanzibar

    (GMT+08:00) 2020-09-24 20:07:53

    Kasi ya mfumko wa bei kwa mwaka uliomalizia August 2020 umeshuka kufikia 2.4% ukilinganisha na 3.6% kwa mwezi wa July 2020.

    Akizungumza na waandishi wa habari Mtakwimu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Salma Saleh Aliy huko katika ukumbi za Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali iliopo Mazizini wakati alipokuwa akiwasilisha mfumko wa bei.

    Amesema chakula na vinywaji visivyo na kilevi vimeshuka kwa kufikia 4.9% August 2020 ukilinganisha 6.7% July 2020.

    Aidha amesema miongoni mwa vyakula vilivyoshuka ni pamoja na mchele wa mbeya , wa pembe , unga wa sembe, ndizi mbichi samaki ,mafuta ya taa , saruji .

    Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Uchumi Tawi la Zanzibar (BOT) Moto Ngwinganele amesema hali iliyosababisha mfumko wa bei kushuka ni chakula kuwepo chakula cha kutosha na kutarajia kuongezeka zaidi.

    Pia amesema kwa upande wa mafuta ya taa, disel na Petrol yameshuka kutokana na kushuka katika soko la dunia kwa kuwepo maradhi ya corona.

    Vile vile amesema kwamba malengo ya Serikali ni kuona wananchi wanaendelea kupata bidhaa kwa bei nafuu ili waweze kujikwamua kimaisha na kumudu kununua bidhaa ambazo zimeshuka katika masoko yote.

    Nao wananchi wamesema wanashukuru Serikali kutokana na kupungua kwa bei na kuweza kumudu kununua chakula..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako