• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jambojet yazindua kampeni ya kuhimiza utalii wa ndani

    (GMT+08:00) 2020-09-24 20:08:15

    Kampuni ya kikanda ya usafiri wa anga ya Jambojet imeshirikiana na baadhi ya mahoteli kukuza utalii wa ndani.

    Kampeni hiyo iliyopewa jina "Now Travel Ready" ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo wa kuhimiza usafiri wa ndege huku nchi ya Kenya ikianza mchakato wa kupona kutokana na makali ya Covid-19.

    Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Jambojet,Titus Oboogi , amesema kuwa kutokana na uzinduzi wa kampeni hiyo,wanataka kuwaonyesha wateja wao kawaida mpya ya kusafiri.Kutoka wakati wanapotoka majumbani mwao,hadi wanapofika uwanja wa ndege,kufika sehemu wanazokwenda,hoteli watakazoishi,pamoja na shughuli ambazo wanaweza kushiriki.

    Hoteli ambazo ni sehemu ya kampeni hiyo ni pamoja na Swahili Beach Resort and Diani Sea Lodge mjini Diani; Ciala Resort, Grand Royal Swiss Hotel na Sovereign Hotel mjini Kisumu; Voyager Beach Resort, Pride Inn Hotels na Hotel Englishpoint mjini Mombasa.

    Shirika hilo la ndege lilirejelea shughuli zake tarehe 15 Julai ikiwa na safari tatu za kila siku kwenda Mombasa,mbili Kisumu,mbili Eldoret,moja Malindi na safari nne kwa wiki kwenda Diani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako