• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitaki "mwalimu wa haki za binadamu"

    (GMT+08:00) 2020-09-24 21:13:06

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, China haitaki "mwalimu wa haki za binadamu", na Marekani inapaswa kuzingatia na kusahihisha masuala yake yenyewe ya haki za binadamu.

    Kauli hiyo imetolewa kufuatia waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kulaani hali ya haki za binadamu nchini China, Iran, Venezuela na nyinginezo.

    Wang amesema serikali ya China inatilia maanani sana kulinda na kuhimiza haki za binadamu, na imefanikiwa kuwasaidia watu milioni 850 kuondokana na umaskini, kukamilisha mifumo mikubwa zaidi duniani ya elimu, huduma za jamii, afya na demokrasia ya kishina, na kulinda uhuru wa raia wake kwa mujibu wa sheria katika kutoa maoni, kuamini dini, na haki ya watu wa makabila madogo kushiriki kwenye utawala wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako