• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa zamani wa Japan akubali pendekezo la rais wa China kuhusu kujenga jumuiya ya pamoja ya afya ya umma ya binadamu

    (GMT+08:00) 2020-09-25 09:08:32

    Aliyekuwa waziri mkuu wa Japan Yukio Hatoyama amesema, anakubaliana na pendekezo lililotolewa na rais Xi Jinping wa China kuhusu kujenga jumuiya ya pamoja ya afya ya umma ya binadamu. Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, Bw. Hatoyama amesema, kuenea kwa virusi vya Corona kote duniani kumetoa onyo kuwa binadamu ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, haiwezekani kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona yanayoweza kutokea tena bila ushirikiano wa kimataifa, pia haiwezekani kuhimiza ufufuaji wa uchumi wa dunia.

    Bw. Yukio ameipongeza China kwa kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya ndani ya virusi vya Corona na kutoa msaada kwa nchi nyingine. Amependekeza kujenga jumuiya ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona ya Asia ya Mashariki, ikiwa ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa pendelezo la rais Xi la kujenga jumuiya ya pamoja ya afya ya umma ya binadamu. Ameeleza matarajio yake kwa China itabadilishana uzoefu na mafanikio yake katika kudhibiti virusi hivyo kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako