• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna wa afya wa EU aonya dhidi ya uchovu unaotokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-25 09:22:25
    Kamishna wa Afya na Usalama wa Chakula wa Umoja wa Ulaya, Stella Kyriakides ameonya dhidi ya uchovu unaotokana na virusi vya Corona unaoonekana katika baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo, wakati hofu ikiendelea kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi hivyo.
    Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video mjini Brussels, Kyriakides amesema baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanashuhudia idadi kubwa ya kesi za virusi vya Corona hivi sasa kuliko wakati wa kilele cha maambukizi hayo mwezi Machi, na baadhi ya maeneo uchovu unaotokana na umbali wa kijamii na kutofuata taratibu za kawaida umeanza kuonekana.
    Amezitaka nchi wanachama kuchukua hatia za haraka mara dalili za mlipuko mpya zinapoonekana, kwani inaweza kuwa nafasi yao ya mwisho kuzuia hali iliyotokea wakati wa majira ya mchipuko kujirudia tena.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako