• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano kati ya China na Afrika waharakisha maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-09-25 17:25:29

    Wakati janga la virusi vya Corona limetoa pigo kubwa kwa uchumi wa Afrika, pia limetoa fursa ya kuharakisha maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani humo. Teknolojia za kisasa na majukwaa yaliyoletwa na kampuni za China vimetoa uungaji mkono kwa Afrika katika kujenga mfumo wa biashara za kielektroniki na kuharakisha mageuzi ya kidijitali.

    Kwenye kipindi cha janga la virusi vya Corona, biashara za kielektroniki zinazokua kwa kasi zimewaonjesha watu wa Afrika manufaa ya mageuzi ya kidijitali. Katika jukwaa la biashara za kielektroniki lililojengwa kwa pamoja na Rwanda na kampuni ya Alibaba, paketi elfu tatu za kahawa ya Rwanda ziliuzwa ndani ya sekunde chache, kasi ambayo imewashangaza watu wa huko.

    Ofisa habari wa Bodi ya Taifa ya Maendeleo ya Uuzaji Nje wa Mazao ya Kilimo nchini Rwanda Pie Ntwali alipohojiwa na Shirika la habari la China Xinhua alisema kuwa katika zama hizi za kidijitali, wanapaswa kujizatiti kwa biashara za kielektroniki, na wamepata fursa ya kuhimiza mageuzi ya kidijitali kutokana na ushirikiano na kampuni ya Alibaba.

    Takwimu zilizotolewa mwezi Agosti na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD zinaonesha kuwa tangu janga la virusi vya Corona litokee, mauzo ya mtandaoni kupitia majukwaa ya biashara za kielektroniki barani Afrika yameongezeka kwa zaidi ya mara moja, na baadhi ya nchi za Afrika zinajitahidi kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa kidijitali kutokana na mapendekezo ya shirika hilo.

    Nchini Kenya, Jukwaa la muziki la Mdundo ambalo limepanua shughuli zake katika nchi 15 za Afrika, limewaleta pamoja wasanii wa Afrika zaidi ya elfu sitini, na mpaka sasa limekuwa na watumiaji zaidi ya milioni tano. Ofisa Mkuu wa Operesheni wa Mdundo.com Vaniko Koinange amesema, idadi ya nyimbo na muziki zilizopakuliwa kutoka kwenye jukwaa hilo imeendelea kuongezeka na kufikia mara milioni 33 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, na kuongezeka kwa asilimia 26 katika robo ya pili ya mwaka.

    Msemaji wa Bodi ya Taifa ya Maendeleo ya Uuzaji Nje wa Mazao ya Kilimo nchini Rwanda Pie Ntwali amesema biashara za kielektroniki zimeonesha mustakbali mkubwa katika bara la Afrika, na zinatarajiwa kuwa njia bora ya kufanya biashara katika siku zijazo. Mkurugenzi wa divisheni ya TEHAMA katika Umoja wa Afrika Moctar Yedaly pia anaona kuwa mageuzi ya kidijitali yana umuhimu mkubwa kwa mustakbali wa Afrika katika siku zijazo.

    Wachambuzi wanaona kuwa, kutokana na majukwaa ya biashara za kielekroniki yaliyojengwa na kampuni za China kwa ajili ya Afrika, na teknolojia za malipo ya mtandaoni na vifaa vya kisasa vilivyotolewa na kampuni hizo, Afrika iko mbioni kujenga mfumo wake wa biashara za mtandaoni.

    Mtaalamu wa Uchumi Jamii wa Zambia Kevin Chisanga amesema Afrika imetambua kwamba ushirikiano kati yake na China unaweza kupunguza gharama za mageuzi ya kidijitali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako