• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UHAMISHO: Sasa ni rasmi Mbwana Samatta ajiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki

  (GMT+08:00) 2020-09-25 17:28:49

  Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England, bado Fenerbahce haijaweka wazi kama wamemsajili kwa mkopo wa msimu mzima 2020/21 kama inavyoripotiwa au ni uhamisho kamili. Fenerbahce wamempa jezi namba 12 Mbwana Samatta ambaye anaenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho, klabu hiyo imewahi kumuwania mara kadhaa hata kabla ya kwenda Aston Villa lakini ndoto ya Samatta ilikuwa ni kucheza EPL. Samatta anaondoka Aston Villa baada ya nafasi yake ya kucheza kuwa finyu sababu Aston Villa wamesajili wachezaji wengine wawili wa nafasi ya ushambuliaji Watkins na Traore, pamoja na Samatta nafasi hiyo ingekuwa na jumla ya wachezaji wanne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako