• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bayern Munich yatwaa kombe la UEFA Super Cup

    (GMT+08:00) 2020-09-25 17:29:06

    Mabingwa wa UEFA Champions League FC Bayern Munich ya Ujerumani wamewaonesha Ubabe Mabingwa wa Europa League klabu ya Sevilla FC kutokea Hispania katika mchezo wa fainali wa UEFA Super Cup. Mchezo huo uliochezwa Budapest Hungary umemalizika kwa FC Bayern Munich kuwa Bingwa wa Kombe hilo kwa kuifunga Sevilla magoli 2-1 mchezo ambao ulilazimika dakika 90 na kwenda dakika 120 ili kupata mbabe. Ushindi huo unaifanya FC Bayern Munich ndani ya mwaka 2020 kuwa imepata ushindi katika mchezo wa 23 mfululizo lakini ni mchezo wao wa 32 wakicheza bila kupoteza na hilo ndio taji lao la nne ndani ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako