• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa barabara mpya inayovuka jangwa kubwa la China wakamilika

    (GMT+08:00) 2020-09-25 19:06:44

    Ujenzi wa barabara mpya inayovuka jangwa la Taklimakan umekamilika na kuweka mazingira ya kuboresha usafiri na ukuaji wa uchumi katika mikoa ya karibu na jangwa hilo kubwa la China.

    Barabara hiyo iliyopo wilayani Bayingolin katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani kusini mwa Xinjiang, inaunganisha kaunti za Yuli na Qiemo. Ni barabara ya tatu inayovuka jangwa la Taklimakan, ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani. Ikiwa na urefu wa km 334, ujenzi wa barabara hiyo umeanza Oktoba 2017, na inatarajiwa kuanza kutumika 2021.

    Barabara hiyo itapunguza umbali kati ya kaunti ya Qiemo na mji wa Korla kwa km 350, na kuchochea maendeleo ya utalii na ukuaji wa uchumi katika mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako