• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UM asisitiza kutafakari masuala ya usimamizi wa dunia na taratibu za pande nyingi kwa njia za kivumbuzi

    (GMT+08:00) 2020-09-25 19:23:15

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana Alhamis alitoa hotuba akitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kutafakari masuala yanayohusiana na usimamizi wa dunia na taratibu za pande nyingi kwa njia za kivumbuzi, ili kukidhi mahitaji ya karne ya 21.

    Katika mkutano wa ngazi ya juu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa dunia baada ya janga la COVID-19 Bw. Guterres alisema kuwa janga hilo ni msukosuko mkubwa wa pande zote ambao umesababisha watu zaidi milioni 30 duniani kuambukizwa na wengine karibu milioni 1 kufariki. Hali hiyo inatokana na upungufu wa maandalizi ya kutosha, ukosefu wa ushirikiano na mshikamano duniani.

    Ametoa wito wa kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto yoyote wakati wowote, pia amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji mtandao wa taratibu za pande nyingi, wenye msingi wa kuimarika kwa mawasiliano na ushirikiano kati ya mashirika ya kimataifa na ya kikanda kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako