• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China akanusha shutuma zilizotolewa na mjumbe wa Marekani katika baraza la usalama la UM

    (GMT+08:00) 2020-09-25 19:23:38

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun jana alitoa hotuba katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa dunia baada ya janga la COVID-19 akikanusha vikali shutuma zisizo na msingi dhidi ya China zilizotolewa na mjumbe wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

    Balozi Zhang Jun alisema kuwa, nchi wanachama wengi wa baraza la usalama zilisisitiza kushikilia mfumo wa pande nyingi na kuimarisha mshikamano na ushirikiano, lakini mjumbe wa Marekani alitoa kauli iliyokwenda kinyume na maoni ya pamoja kwenye mkutano huo. China inapinga na kukataa shutuma za Marekani zisizo na msingi wowote.

    Mbali na hapo amesema, Marekani inapaswa kutambua kuwa kuzilaani nchi nyingine hakusaidii kutatua masuala yake yenyewe, bali ni kwenda mbali zaidi katika njia ya makosa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako