• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 16 wakamatwa na polisi 9 kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga zuio mjini London

    (GMT+08:00) 2020-09-28 08:41:17

    Polisi ya jiji la London imesema watu 16 wamekamatwa na maafisa tisa wa polisi wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea kwenye maandamano ya kupinga zuio katikati mwa London.

    Kwa mujibu wa gazeti la Evening Standard, maelfu ya watu walikusanyika kwenye uwanja wa Trafalgar siku ya Jumamosi na kubeba alama, bendera na mabango mbalimbali na kushiriki kwenye mkusanyiko waliouita "hatujaridhia". Hakuna mwandamanaji hata mmoja aliyevaa barakoa au kufuata kanuni ya umbali wa kijamii.

    Maafisa wa polisi walipambana na umati wa watu wakati wakijaribu kuzuia mkusanyiko kutokana na kutofuatwa kwa kanuni za umbali wa kijamii, ambapo watu walirusha chupa na polisi kutumia virungu, na kusababisha baadhi ya waandamaji kujeruhiwa. Polisi ya London imesema imekuwa ikishauriana na waandamanaji kwa wiki nzima ili kuwakumbusha wajibu wao wa kisheria na kuwaelezea kuwa tukio hilo linaweza kukiuka kanuni za virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako