• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la biashara huria la China na ASEAN lahimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili

    (GMT+08:00) 2020-09-28 09:26:04

    Msaidizi wa waziri wa biashara wa China Bw. Li Chenggang amesema, eneo la biashara huria la China na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) limekuwa eneo la biashara huria lenye nguvu ya uhai zaidi duniani.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Bw. Li amesema, tangu eneo hilo lianzishwe miaka kumi iliyopita, limehimiza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji kati ya China na jumuiya ya ASEAN, mwaka 2019 thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imefikia dola za kimarekani bilioni 641.5 kutoka dola za kimarekani bilioni 292.8 za mwaka 2010. Mwaka huu jumuiya ya ASEAN imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako