• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Azerbaijan atangaza nchi yake kuingia kwenye hali ya vita

    (GMT+08:00) 2020-09-28 09:27:52

    Rais Ilham Heydar oglu Aliyev wa Azerbaijan jana alitoa amri ya kutangaza hali ya vita, na kutekeleza marufuku ya kutotoka nje usiku nchini kote kuanzia leo tarehe 28 kwa saa za huko.

    Mapambano mapya kati ya Azerbaijan na Armenia yametokea jana kwenye eneo la Nagorno-Karabakh, ambapo kila upande umelaani upande mwingine kwa kukiuka usitishwaji vita na kufanya mashambulizi kwanza.

    Naye msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa jana alitoa taarifa akisema, katibu mkuu wa umoja huo Bw. Antonio Guterres anafuatilia mapambano kati ya Azerbaijan na Armenia, na kuzitaka pande hizo mbili zisitishe mapambano mara moja, na kurejesha mazungumzo yenye maana. Amesema atafanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Azerbaijan na waziri mkuu wa Armenia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako