• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maajabu kwenye ligi ya Ujerumani Beyern yachapwa 4-1 na Hoffenheim

  (GMT+08:00) 2020-09-28 16:26:26

  Katika hali ya kushangaza wengi klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi, na bingwa wa kombe la klabu bingwa, wamefungwa magoli manne kwa moja katika mchezo wa kushangaza wengi, baada ya kutoshindwa katika jumla ya mechi 32 tangu mwezi Desemba mwaka jana. Dalili za mvua zilianzia kuonekana mapema baada ya Ermin Bicakcic kuwaweka wenyeji klabu ya Hoffenheim mbele katika dakika ya 16. Dakika nane baadaye kosa la beki wa Bayern, Benjamin Pavard lilimruhusu Munas Dabbur kumpiga chenga na kucheka na nyavu. Bayern, ambayo iliifunga Sevilla katikati ya wiki kwenye mechi za Uefa Super Cup, ilionyesha dalili za uchovu wakati wenyeji wakiendelea kushinikiza na Kramaric akafunga goli la ushindi katika dakika ya 77. Mshambuliaji huyo wa Croatia alidhibiti krosi na akageuka vizuri kabla ya kumpiga chenga tena golikipa Neuer. Pamoja na kuwa kuna madai ya uchovu, ukweli ni kwamba Bayern ilionekana kulemewa katika muda wote wa mchezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako