• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Luis Suárez aanza kwa ushindi katika klabu ya Atlectico Madrid

  (GMT+08:00) 2020-09-28 16:26:55

  Nchini Hispania baada ya vuta nikuvute kati ya klabu ya Barcelona na Messi na Luis Suárez, wachezaji hao sasa wanaonekana kuwa nje, na mmoja wao tayari ameanza kufanya vitu vyake. Jana Luis Suárez aliyehamia katika klabu ya Atlético Madrid alitumia mchezo wake wa kwanza akiwa amekaa kwenye uwanja Wanda Metropolitan ukiwa mtupu akiwatazama wachezaji wenzake wapya wakipambana na klabu ya Grenada. Kocha ambaye aliamua kumuingiza Suarez wakati klabu yake inaongoza kwa magoli matatu kwa bila, zikiwa zimebaki dakika 20 tu za mchezo hakushangaa kuona Suárez akitikisa nyavu mara mbili, katika mchezo ulioishia Atletico kushinda kwa magoli 6 kwa moja. Nusura Suárez apate hat-trick baada ya shuti lake kugonga mwamba. Katika hali ya kushangaza mchezaji wa Ureno anayeonekana kuwa mbadala wa Lionel Messi kwa Suárez kama angeendelea kuwa Barcelona, aliweza kushirikiana vizuri na Suárez na inaonekana wawili hao wanaweza kuwa pacha wazuri kwenye safu ya mashambulizi. João Félix ni kijana ambaye ameonekana kuwa na kasi kumchezesha vizuri Suárez.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako